Thursday, March 15, 2012

MASKINII !! KAJALA KIFUNGONI !!

Aliyewahi kuwa Mrs. Majani, malkia wa Bongo Records na sasa Bongo Movie actress Kajala Masanja, mapema leo amechukuliwa na kufungwa Segerea kufuatia mashitaka ya ufujaji wa pesa za umma zinazomkabili yeye pamoja na mume wake wa sasa hivi. Kesi hiyo ambayo imekuwa ikisikilizwa kwa muda mrefu sasa inaonekana kufikia hatua za mwisho baada ya hakimu kusemekana kutoa hukumu Jumatatu ya tarehe 19 Machi mwaka huu. Kajala ambaye ana mtoto na P-Funk, hivi sasa yuko Segerea akisubiri hukumu yake kusomwa baada ya siku hizi chache. Washikaji zake wametoa tamko mbalimbali kupitia blogs, BBM na Facebook za kumuombea uzima na uwezo wa kuepuka kifungo. Mimi pamoja na wadau wote wa sanaa tunampa pole KAJALA,kwa matatizo yote yaliyotokea

No comments:

Post a Comment