Sunday, March 11, 2012

MAUAJI YA KUTISHA MKOANI MBEYA MWANAMKE AKATWAKATWA NA MAPANGA, MWINGINE APIGWA RISASI NA MMOJA ACHOMWA KISU CHA TUMBO KISA REDIO AINA YA RISING YA SHILINGI 16,000/=

Mwili wa Marehemu Tabu Bakari Mwangela (58), ukiwa umeharibika vibaya baada ya kukatwakatwa na mapanga na mtu au watu wasiofahamika katika Kijiji cha Malamba wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Ndugu wa marehemu wakilia baada ya kuuona mwili wake Tabu Bakari Mwangela (58), aliyeuawa kwa kukatwakatwa na mapanga na mtu au watu wasiofahamika katika Kijiji cha Malamba wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Waombolezaji katika msiba wa marehemu Tabu Bakari Mwangela (58), aliyeuawa kwa kukatwakatwa na mapanga na mtu au watu wasiofahamika katika Kijiji cha Malamba wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Watu watatu wamefariki dunia mkoani Mbeya kwa matukio matatu tofauti yaliyotokea Machi 7, mwaka huu likiwemo tukio la mtu kipigwa risasi, kukatwakatwa na mapanga na jingine la kuchomwa kisu tumboni. Tukio la kwanza limetokea Kijiji cha Kongoro Mswisi, Kata ya Mswisi ambapo mwananchi mmoja aitwaye Adam Jason Mwajeka (25), ameuawa kwa kupigwa risasi tumboni na watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi Februari 7, mwaka huu majira ya saa mbili usiku baada ya majambazi hao kuvamia baadhi ya maduka na kupora pesa za mauzo katika maduka kadhaa. Majambazi hao waliokuwa na silaha walianza kwa kumzuia mwanamke anayefahamika kwa jina la Tumpale Ally (32), ambaye ni mke wa Milele Kaponda kisha kumpora pesa za mauzo shilingi milioni 2 za kitanzania, mita chache kabla ya kuingia nyumbani kwake. Wakati wakibishana mwanamke huyo alimuita mumewe na alipojaribu kutoka kumsaidia, majambazi hao walifyatua risasi mbili hewani Tumpale aliachia pesa hizo kunusuru uhai wake. Haikuishia hapo majambazi hao walivamia duka la Leonard Edwin Mwampyate (34), na kupora pesa shilingi milioni tatu na laki tano, pamoja na simu ya mkononi aina ya Nokia yenye thamani ya shilingi elfu themanini na tano, pia dukani alikuwepo nduguye Goliath Mwangonji ambaye walimwamuru kutoa pesa kutoka mfukoni ambapo walimpora shilingi lakini mbili na elfu ishirini. Aidha waliingia duka jingine linalomilikiwa na Bwaba Luka Mwasamaki na kupora shilingi elfu sabini na walipokuwa wakitoka, walimfyatulia risasi Adam Mwajeka tumboni na kufariki papohapo na katika harakati za kujiokoa Elimu Konga (32), alipigwa risasi ya mguu na majambazi hao wakapata nafasi ya kutokomea gizani. Miongoni mwa watu walionusurika katika tukio hilo ni pamoja na Diwani wa Kata hiyo Bwana Furgence Mhegele na Askari wa usalama wa barabarani aliyetayetambuliwa kwa jina moja la Salehe, na mazishi ya Adam yamefanyika kijijini hapo huku Bwana Eliamu amelwanzwa katika Hospitali ya Chimala Mission. Tukio la pili limetokea Kijiji cha Malamba wilaya ya Mbarali mkoani hapa, Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Tabu Bakari Mwangela (58) ameuawa kwa kukatwakatwa na mapanga na mtu au watu wasiofahamika. Mwili wa marehemu umegunduliwa baada ya watu waliokuwa na ahadi ya kuuziana shamba kumsubiri kwa muda mrefu shambani kwake, ndipo walipoamua kumfuata nyumbani kwake na kukuta mlango ukiwa wazi, wakijua marehemu hayupo mbali ndipo walipomuuliza jirani yake aitwaye Devotha Jeremia, na kudai hafahamu alipo. Watu hao waliamua kugonga dirisha bila mafanikio yoyote na ndipo waligusa mwili wa marehemu kwa kwa kupitisha mkono dirishani na kuamua kumuita nduguye aitwaye Matrida Matiya (59), alipoingia nadni alikuta marehemu akiwa juu ya kitanda chake ndani ya chandarua na alipopenyeza mkono alikutana na damu kwenye kiganja na ndipo alipogungua kuwa nduguye kauawa. Bi Matrida alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Balaza la Kata Bwana Peter Elias Sankala, ambaye naye alitoa taarifa kwa mwenyekiti wa Kijiji Ngumbushe Mwalyego na kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Igurusi ambao walifika eneo la tukio na kufanya uchunguzi wa mwili wa marehemu kwa kumtumia Daktari na kuukabidhi kwa ndugu na mazishi kufanyika kijijini hapo. Hata hivyi hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusika na matukio yote mawili na Jeshi la Polisi bado linaendelea kufanya uchunguzi ili kuweza kuwabaini wahusika. Wakati huohuo Mwakingili Mwakaji anashikiliwa na Jeshi la Polisi, baada ya kutuhumiwa kusababisha kifo cha Elias Mwalyego (37), baada ya kumchoma kisu tumboni na kufariki papo hapo katika Kijiji cha Itimba wilaya ya Chunya mkoani Mbeya. Chanzo cha kifo hicho ni marehemu kwenda nyumbani kwa mtuhumiwa kudai rediuo yake aina ya Rising yenye thamni ya shilingi 16,000 za kitanzania, ndipo mtuhumiwa aliingia ndani huku marehemu akidhani mtuhumiwa kaenda kumchukulia redio yake badala yake alitoka na kisu na kumchoma marehemu tumboni na kufariki. Diwani wa Kata ya Itimba Bwana Michael Zanzi amesema marehemu amesafirishwa kuzikwa eneo la Mbalizi. Kwa upande wa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amethibisha matukio yote matatu. Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.