Saturday, April 7, 2012

BREAKING NEWS,MSANII KANUMBA KAFARIKI DUNIA




Taarifa tulizozipata sasa hivi, ni kwamba kweli mwigizaji STEVEN KANUMBA amefariki dunia na inaaminika chanzo cha kifo chake ni baada ya kuanguka na kuanza kutoa mapovu hapohapo nyumbani kwake, alikua akiishi na mdogo wake anaitwa Fetty aliekua chumba kingine ambae amethibitisha kweli kwamba alimkuta kaka yake akiwa ameanguka.

Polisi wameondoka nyumbani kwa Kanumba muda mfupi uliopita baada ya kuwachukua waliokua wanaishi na Kanumba akiwemo mdogo wake Fetty ili kwenda kusaidia maelezo ya kilichotokea.

Bado watu wanazidi kuongezeka nyumbani kwa Kanumba ambapo tayari idadi kubwa ya wasanii wenzake wamefika pamoja na watu mbalimbali.

Ila kumekua na taarifa nyingine ambazo hazijathibitishwa kwamba Kanumba alianguka na kuumia kichwani baada ya mpenzi wake kumsukuma na kuanguka wakati wanagombana.

No comments:

Post a Comment