HII BARUA KUNA MSICHANA KANITUMIA,ANAHITAJI MSAADA WA KIMAWAZO JAMANI!! NAOMBA TUMSAIDIE IKIWEZEKANA,MM NAIWEKA KM ALIVYONITUMIA YY BILA KUONGEZA KITU WALA KUPUNGUZA.ALIANZA HIVI !!!!
Habari dada Shumy,mm ni binti wa miaka 23.Nasumbuliwa sana na mapenzi hadi sijielewi.Tatizo langu ni moja,4 yrs ago niliingia kwenye ulimwengu wa kimapenzi na kijana mmoja aliyenipenda kupita kiasi,sasa ikatokea yeye ameenda nje kusoma,mimi huku shetani akaniingia nikapata boyfriend mwingine nikajikuta namdelete Yule wa mwanzo bila kosa lolote.nikiwa na huyu wa sasa kasheshe ndio ikaanza.nampenda kupita kiasi huyu kaka ila yeye haeleweki,umri wake ni 25 yrs.story ni ndefu naomba niishort.nimekuwa msaada mkubwa kwake kuanzia kumfulia,kumpikia hadi kumuhudumia ingawa sio kivile ila nikipata pesa huwa nampigisha pamba za uhakika na pesa zangu huwa anazishika yeye,lakini tofauti nayeye hana huo muda wa kuninunulia chochote.nimeshamtambulisha kwetu wote wanamjua ila yeye hataki kunitambulisha kwao eti bado wanafunzi wakati tayari tupo chuo.profile yangu ya FB nikiweka picha zake ananiambia nizitoe hakuna haja ya kujishow off na hata kule kwake hajaweka za kwangu.yote hayo namvumilia kwasbb nampenda mno.wakati mwingine namkumbuka EX wangu alikuwa na mapenzi ya kweli kwangu,ila huyu wa sasa yeye hanidekezi ni amri kwa kwenda mbele,anachosema/anachotaka yeye ndio hicho hicho mimi sina say yoyote.sometimes nahis kama ana GF mwingine zaid yangu au kama mimi ndio ninayejipendekeza kwake.Tatizo lililonifanya niandike hii habar ni kuwa,hivi sasa mimi ni mjamzito na kwetu wameshajua wamesema wanataka wamuone muhusika,ila yeye hataki kusikia hizo habari na ameniambia niitoe eti kwa kuwa haya masomo tunayosoma sisi ni magumu sana atashindwa kunihudumia ipasavyo yeye hataki lawama.wakati tumeshatoa mimba mbili tayari nikamwambia hii sitaitoa kamwe.from there hana story na mimi kabisa.ila akipiga simu ananiuliza kama nishaitoa au bado.amesema bado ananipenda sana,tumalize chuo kwanza mambo mengine baadae.sasa nipo njia panda sijui nifanyeje,jee huyu BF anania njema na mimi kweli au ananitumia tuu???
No comments:
Post a Comment