Tuesday, May 22, 2012
JULIO AMEWAJIA JUU WASANII WA BONGO MOVIE !
Kocha wa timu ya Coastal Union ambaye pia ni Kocha msaidizi wa timu ya vijana ya taifa chini ya miaka 20 Ngorongoro Stars na aliyewahi kuwa mchezaji wa zamani wa klabu ya Simba Pamoja na Taifa Stars, Jamhuri Kihwelu jana usiku alisikika akiwalalamikia wasanii wa filamu na wasanii wa Bongo Flava dhidi ya kitendo chao cha kutoonekana katika msiba wa mchezaji marehemu wa Simba SC Patrick Mafisango.
Kocha Jamhuri Kihwelo ambaye anajulikana zaidi kama Julio, alisikika katika viwanja vya Leaderz akiwalalamikia wasanii wa filamu za vichekesho yaani Komedi, msanii Steve Nyerere, pamoja na Masanja mkandamizaji kwa kitendo cha wanatasnia ya Filamu ama Bongo movie na wasanii wa bongo Flava Kwa ujumla kwa kutoonekana kwenye msiba wa Mchezaji Mafisango.
Aidha Julio alihoji kwamba inakuaje kwamba wasanii, wadau na wapenzi wa filamu na bongo flava kutoonekana wakati wachezaji, pamoja na wadau mbali mbali wa tasnia ya mpira wa miguu walishiriki kikamilifu katika shughuli yote ya msiba wa marehemu Steven Kanumba kuanzia siku ya kwanza hadi siku ya mazishi.
Akiongea kwa hisia kali, Julio alimwuuliza steve Nyerere, “Wewe kwa nini haukutokea wala kupeleka ubani wakati wa msiba, inamaana hamkuwa hata na mtu wa kuwawakilisha?” Julio aliendelea kumwambia yeye steve na mwenzake Irene Uwoya wameenda hadi kutengeneza kaburi upya la Kanumba kama sehemu ya kutafuta sifa wakati mwili ulishazikwa.
Akiendelea Julio ambaye amezoeleka sana kwa utani na mashara alimfuata Masanja na kumpa maneno hayo hayo aliyomwambia Steve Nyerere,na pia kumgeukia Asha Baraka ambaye naye alimsihi Julio kuwasamehe. Julio alisema amesikitishwa sana na namna wasanii hao wasivyokuwa na ushirikiano kwa kuwa wanaona sasa wamepata jina.
“ Hii si haki kutoka kwa hawa wenzetu kususia mazishi ya Mafisango”
Katika kukazia maneno Julio alimwambia Steve Nyerere, “Mbona wewe ulilia kuliko ndugu wa Kanumba na alipokuja Raisi Kikwete ukajitupa kabisa chini kuonyesha umeguswa sana ama ilikuwa janja ya nyani kuonyesha una uchungu wakati huku kwingine hutaki kutokea ama hauna uchungu na wadau wa mpira.”
No comments:
Post a Comment