Amini usiamini lakini ukweli ni kwamba msanii wa muziki wa kizazi kipya, Amini Mwinyimkuu ‘Amini’, yuko kwenye maandalizi ya kutoa ngoma mpya ambayo atamshirikisha laaziz wake wa zamani Linah.
Amini na Linah walikuwa wapenzi lakini walikuja kuachana na siri ya kuachana kwao wanaijua wenyewe.
Amini ambaye ambaye kwa sasa yuko bize na ngoma hiyo, alidai kuwa kutoka na mawazo ya watu kuwa yenye ana chuki na Linah, sasa ameamua kumshirikisha katika ngoma yake ili kuweka wazi na kufuta kauli za watu wenye nia mbaya.
Wakati amini akisem ahayo, Linah yeye amedai kuwa ameamua kufanya ngoma moja na Amini, kwani wao ni wasanii na wanahaki ya kushirikiana.
No comments:
Post a Comment