Habari zilizotufikia hivi punde toka vyanzo vya uhakika ni kuwa meli inayofanya safari zake kati ya Zanzibar na Dar iitwayo Mv. Skaget imezama baada ya kushindwa kuhimili mawimbi makali.
Inasemekana kuwa meli hiyo iliyokuwa imebeba abiria zaidi ya 200 ilipata dhoruba hiyo eneo la Chumbi. Hata hivyo vyombo vya kuokoa viko njiani kuelekea kwenye eneo la tukio.
Hapa Dar, kulikuwa na upepo mkali sana leo mchana.
Tutaendelea kuwahabarisha.
No comments:
Post a Comment