GARI ZENYE PLATE NUMBER ZA JINA LA MUHUSIKA,ZAANZA KUTUMIKA TANZANIA
MAMLAKA ya mapato nchini (TRA) imetangaza kuanzishwa kwa mfumo mpya wa usajili wa namba binafsi za magari (personalized number plate) ambapo wenye magari wanaweza kutumia jina au neno lolote wanalochagua badala ya namba za kawaida.
Kwa mujibu wa matangazo yaliyotolewa na mamlaka hayo katika vyombo vya habari, wamiliki wa magari watakaotaka kutumia namba hizo wameshauriwa kupeleka maombi kwenye ofisi za TRA zinazohusika na usajili wa magari zilizopo katika mikoa yote Tanzania Bara.
Likifafanua zaidi utaratibu huo, tangazo hilo limeeleza kwamba kabla ya gari kupewa namba binafsi ni lazima kwanza lisajiliwe kwenye mfumo wa namba za kawaida, na kwamba namba binafsi ni lazima iwe ni jina la mtu, kampuni au neno lililochaguliwa na mwombaji.
Masharti mengine ni kwamba namba binafsi lazima iwe na herufi kuanzia mbili hadi kumi, na kwamba namba ikishatolewa kwa gari moja haiwezi kutolewa kwa gari jingine. Vilevile, muda wa kutumia namba binafsi iliyosajiliwa ni miaka mitatu na mhusika akipenda kuendelea na utaratibu huo atalazimika kulipia tena.
Gharama ya usajili wa namba hizo ni Sh. 5,000,000.
Hivi karibuni, sheria ya usajili wa namba binafsi za magari ilipitishwa na bunge.
No comments:
Post a Comment