Sunday, July 22, 2012

HATIMAE MTOTO WA KAMBO WA USHER RAYMOND AFARIKI DUNIA



Kyle Glover ambae ni mtoto wa mke wa zamani wa Mwimbaji Usher Raymond, amefariki dunia leo kutokana na kuumia kwenye ajali ya pikipiki za kwenye maji maarufu kama Jetski mwanzoni mwa mwezi huu huko Georgia Marekani.
Madaktari wametoa mashine zilizokua zinasaidia kumuweka hai mtoto huyo aliekua na umri wa miaka 11 baada ya kugundua kwamba majeraha aliyoyapata yasingeweza kutibika.
Kyle akiwa na rafiki yake wa kike mwenye umri wa miaka 15 walipata ajali july 8 2012 huko Georgia baada ya Inner tube waliyokuwemo iliyokua ikivutwa na boti kugongwa na Jetski wakiwa kwenye maji na hivyo kupata majeraha ya kichwa.

No comments:

Post a Comment