Msanii wa Filamu nchini, Jaqueline Wolper, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, kuhusu pambano lake la ngumi na mpinzani wake, Wema Sepetu.
Pambano hilo ambalo litakuwa la raundi 6 litakuwa ni mojawapo ya mapambano ya utangulizi kusafisha njia kwa mabondia Francis Cheka na Japhet Kaseba.
Wolper amesema anaendelea kujifua ili kuhakikisha kwamba mpinzani wake(on and off stage) hatoki ulingoni bila “mchuzi”. Hayo yote yatajiri Uwanja wa Taifa siku ya Jumamosi 7/7/2012..Saba Saba.
No comments:
Post a Comment