Monday, July 9, 2012
SOMA KUJUA ASHA BARAKA ALICHOKIANDIKA KATIKA PAGE YAKE YA FACEBOOK LEO ZIDI YA MASHUJAA BAND
Mimi ni Mdau mkubwa sana wa Muziki kwa kuwa nipo muda mrefu sana katika Tasnia hii ya Muziki wa Dansi hivyo basi nina haki na wajibu waa kutoa mchango wangu kupitia vyombo vya habari kwa kuwa hakuna sanaa isiyoonekana sanaa ni ile inayoonekana. Kwa nini nijifiche wakati mimi ni mtu mwema ndani ya jamii. Ni imani yangu wanaojificha au wanaosemea pembeni si watu wema.
Msemaji wa Mashujaa Hosea au kwa Jina lingine maarufu Maisha ni mtu ambaye si mzoefu sana katika uendeshaji wa Bendi ndio maana ni mara nyingi amekuwa akishauriwa vibaya juu ya uendeshaji wake kwa kumuona ‘Bwege’. Miziki ni mipango wala si majungu.
Hosea au Maisha kwangu mimi namchukulia kama ni Rafiki mnafiki kwa kuwa alianzisha biashara baada ya kuniona mimi nafanya Biashara hiyo.
Nataka nimhoji Mafundi wawili aliowafukuza ambao ni Robi na Mapunda aliwachukulia wapi kama si Twanga Pepeta? Ibrahim (Mirinda Nyeusi) ni mimi ndiye niliyemleta toka South Africa Mwaka 2007. Hata huyo Meneja wake King Dodoo mimi ndiye niliyemleta hapa Nchini.
Niongeapo huwa nina maana kubwa sana kwa kuwa kama umefukuza watu halafu wewe huyo huyo unaenda kuwachukua mafundi wote wa Msondo una maana gani hapo kama si uongo huo na unafiki hao wafanyakazi wako unaowatuma wakome mara moja kwani wao kwenye Radio walikuwa wanaongea nini.
Kama kweli wewe Mwanaume Jabali mwenye kipato halali kwa nini ujifiche? Wakurugenzi na wamiliki wote wa Taasisi maarufu huwa wanaonekana mbele ya Jamii kwa nini na wewe usionekane kama wenzio tunavyoonekana?
Mimi nitakuelekeza unapokosea sio leo tu siku zote. Matusi yako ya kutaka eti kuniajiri mimi ukome kwa kuwa mimi siwezi kuajiriwa na pesa CHAFU naajiriwa na pesa zilizokuwa safi. Nimefanya kazi Shirika la Umma kwa miaka 30 sikufukuzwa wala kuiba hata senti moja. Mimi ni mtu safi.
Endapo ukinivunjia heshima yangu niliyoijenga kwa muda mrefu ndani ya Jamii nami nitakuvunjia, sikuogopi na mkome kunifuatafuata na kunivunjia heshima kupitia kwenye Facebook. Uliwahi kuandika kuniandika kwenye Mtandao wa Ze Utamu naona unataka kurudia ili kupata umaarufu.
Kama ungekuwa na pesa ungekesha kuuza pombe Mashujaa Pub na kupigizana kelele. Wenye pesa wanapumzika. Jiulize umetumia ngapi na umerudisha ngapi. Unataka umaarufu na kupandisha Bendi yako kupitia Twanga na ndio maana hata Fundi Mitambo, Meneja wote unachukua Twanga ili upate umaarufu. Umaarufu unakuja kwa kazi nzuri na ya muda mrefu.
Nitawakosoa kila kukicha nitapoona kuna ulazima wa kufanya hivyo. Jana mmediriki kupitisha PA sehemu tunayopiga mchana ili mradi kutufanyia fujo tu sas sijui mlfuata nini kama si fujo na sisi tukija sehemu yenu je?
Mmediriki kuzuia wanamuziki wa Twanga Pepeta kuingia kwenye onyesho lenu Dodoma.
Hivi aibu huna wewe Kaka Rafiki adui. Sikupendi kwa tabia chafu jirekebishe.
Nimeamua kujibu kwa njia hii Facebook badala ya nyinyi kuitumia njia hii tofauti na kawaida yenu ya kutumia mikutano ya waandishi wa habari na kwenye Interview kupitia Vituo vya Redio na Tv mbalimbali.
No comments:
Post a Comment