Monday, July 23, 2012
WALI WA SHEREHE WAUA MMOJA, 40 WALAZWA IRINGA
Wagonjwa wengine walioathirika na chakula hicho wakiwa wodini.
MTU mmoja mkazi wa kijiji cha Ibofye wilaya ya Kilolo mkoani Iringa aitwaye Wagila Nyaupumba, amefariki dunia na wengine zaidi ya 40 wamelazwa katika hospitali mbalimbali za mkoa wa Iringa kikiwemo kituo cha afya cha Ipogolo na Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa baada ya kula wali na kunywa togwa vinavyosadikika kuwa na sumu katika shehere ya kutoa mahari.
Tukio hilo lilitokea juzi Jumamosi baada ya mkazi wa kijiji hicho, James Ngaile, kuandaa chakula na kinywaji hicho kwa kwa ajili ya sherehe ya kuoza binti yake.
Habari zilizopatikana zinasema baada ya kula chakula hicho na kufika nyumbani usiku, waathirika walianza kuharisha damu na baadaye kukimbizwa hospitali ambapo marehemu alifariki na wengine hali zao zinaendelea vizuri.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamhanda, alipoulizwa na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu jana kuhusu tukio hilo alisema bado halijafika ofisini kwake na kuwa pindi litakapomfikia atalitolea ufafanuzi.
Na Francis Godwin, Iringa
No comments:
Post a Comment