Monday, August 20, 2012
MASHUJAA BAND CLASSIC KUWAPA RAHA WAKAZI WA MTWARA IDDI PILI
Naye Meneja wa Bendi hiyo Martin Sospeter alisema kwamba, siku ya Idd Mosi walikuwa Msasani ndani ya Ukumbi wa Emirates, na kwa upande wa Idd pili ni zamu ya wakazi wa Mtwara Mjini ndani ya Ukumbi wa Makonde Beach ili kuwapa radha wakazi wa huko.
Hiyo yote ni Baada ya kukamilisha ziara ya kuwaanika wanamuziki wake wapya, Bendi hiyo ya Mashujaa ikiwa imejipanga kuwapa burudani wapenzi wake siku ya Iddi Mosi na Iddi Pili.
Kwa sasa Bendi hiyo ipo chini ya Rais wake Charl Baba, itafyatua burudani hiyo kwa dhumuni la kutangaza kazi zao mpya kwa wapenzi wa burudani hiyo.
Charl Baba alisema kwamba kwa wale wanaoisikia Mashujaa kwenye vyombo vya habari, sasa ndiyo wakati wao wa kuiona bendi hiyo ‘laivu’ katika sherehe za Idd el Fitri.
No comments:
Post a Comment