Monday, September 10, 2012

MWASITI ATENGENEZA NYIMBO MPYA NA PRODUCER WA AKON


Zamani wengi tulikuwa tukimwona kama binti mdogo, lakini hivi sasa naweza kusema ni mdada mkubwa haswaa, huyu si mwingine bali ni Mwasiti Almasi ambae kwa sasa anafanya vizuri sana na pini lake MAPITO.

Akiongea kwa njia (SMS) wikiendi iliyoisha, mdada huyu ambaye ni zao la nyumba ya vipaji ya (THT) ameweka wazi kuwa amefanya ngoma na producer mkubwa marekani anaeitwa Hakeem.

Kwa taarifa yenu tu ni kwamba Hakeem ameshawahi kufanya ngoma na wakali kibao duniani akiwemo Akon kwenye pini (i wanna be with you),ameshafanya na Youssu ndor na wakali wengine kibao.

"Nimefanya nae ngoma mbili moja ikizungumzia wanawake na matatizo yanayowakuta, ila ya pili ipo kibongo fleva zaidi, nimefurahi sana na naiheshimu sana kazi yangu."

No comments:

Post a Comment