Mwimbaji Mkongwe wa Bendi ya Msondo Ngoma, Mzee Muhidini Gurumo kushoto akiimba sambamba na Hassan Moshi 'Tx Jr' wakati bendi hiyo ilipotumbuiza katika ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni. Mzee Gurumo ni mwanamuziki mkongwe pekee aliyedumu katika Jukwaa kwa muda mrefu nchini ambapo hivi karibuni alikuwa akisumbuliwa na maradhi yanayomkabili lakini kwa sasa karudi ulingoni kukonga mashabiki wa bendi hiyo. Msondo kila Jumapili inatumbuiza katika ukumbi wa Max Bar.
Waimbaji wa Bendi ya Msondo Ngoma wakitoa burudani wakati walipokuwa wakitumbuiza katika ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni kutoka kushoto ni Mzee Muhidini Gurumo, Hassan Moshi na Shabani Dede.
No comments:
Post a Comment