Monday, October 15, 2012

RATIBA YA MAANDALIZI YA MAZISHI YA ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA, LIBERATUS BARLOW

Kamati ya maandalizi ya mazishi ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Liberatus Barlow, kwa niaba ya Inspekta Jenerali wa Polisi, inapenda kuwajulisha wananchi wote utaratibu wa mazishi utakavyokuwa kuanzia mwili kuagwa Mkoani Mwanza, Dar es Salaam na kuzikwa nyumbani kwao Mkoani Kilimanjaro. Jumapili tarehe 14/10/2012 mwili wa Marehemu utaagwa Mkoani Mwanza. Jumatatu tarehe 15/10/2012 mwili wa Marehemu utasafirishwa kutoka Mwanza kuelekea Dar es Salaam nyumbani kwake Ukonga. Jumanne tarehe 16/10/2012 mwili utaagwa nyumbani kwake Ukonga Jijini Dar es Salaam na baadae kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Mkoani Kilimanjaro kwa mazishi yatakayofanyika Jumatano tarehe 17/10/2012. Taarifa zitaendelea kutolewa mara kwa mara kadiri ya mipango itakavyokuwa inaratibiwa katika kila Mkoa mwili utakapofika. Imetolewa na: Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu

No comments:

Post a Comment