Tuesday, November 6, 2012
KUTOKA KATIKA GAZETI LA UDAKU SPESHO !!
Mtoto mduchu anayefanya Bongo Fleva, Nasib Abdu Juma ‘Diamond’, alianza kung’ara mwaka 2010 pale aliponyakua tuzo tatu za Kili Music Awards na baada ya hapo, alijihesabu kuwa staa, hivyo kula sahani moja na mastaa ambapo sasa matokeo yanaelekea kumfelisha kimuziki.
Jumamosi iliyopita, Diamond alifanya shoo kwenye Fainali za Miss Tanzania 2012-2013 na jinsi alivyoonesha uwezo mdogo siku hiyo, wadau walinena kwamba kijana ameanza kufeli kimuziki, ule uhodari wake wa kucheza na jukwaa umepotea.
Diamond akipondwa na kushushwa hadhi, nyuma yake kuna maneno kuwa chanzo cha uwezo wa dogo huyo kushuka ni mapenzi na mhusika mkuu ni Wema. Ipo wazi kwamba Diamond na Wema wameshindwa kuachana licha ya kutangaza kufanya hivyo mara nyingi.
HUU NDIYO MWANZO WA MWISHO WA DIAMOND?
Mwanzo wa mwisho ni msemo kutoka kwenye maneno ya Kiingereza, The beginning of the end. Hoja ni kwamba kiwango kidogo alichokionesha Diamond kwenye jukwaa la Miss Tanzania ni ashirio baya kuwa huenda ndiyo mwanzo wa mwisho wake kutamba kimuziki.
Kilichoonekana siku hiyo ni kwamba Diamond hana jipya na zaidi ameanza kuwa mzito jukwaani. Amekosa ubinifu wa kumfanya shabiki amuone wa tofauti. Amebaki yuleyule, hivyo biashara yake inaelekea ukingoni.
Kwa macho rahisi unaweza kutoa kauli kwamba Diamond amebweteka au amelewa sifa lakini ukweli ubaki kwenye mstari kwake kuwa penzi la Wema ni kilevi kikali kwake ambacho kwa kasi ya ajabu kinampotezea dira.
Diamond baada ya kulewa mapenzi ya Wema, sasa amegeuka sokomoko au pampula. Na kwa sababu ‘bwa mdogo’ huyo asili yake ni Kigoma, kule mlevi huitwa mboregwa, kwa hiyo binti wa Balozi Isaac Sepetu, amemfanya staa wa wimbo wa Mbagala awe mboregwa wa mapenzi.
Kama zamani alipokuwa anafanya shoo, watu walikuwa hawakai, wanacheza na kumiminika jukwaani kumtuza, siku hiyo aliimba wapi! Akateremka kuwafuata mashabiki walipo lakini hakuna aliyesimama wala kuonesha kusisimkwa na shoo yake. Napigia mstari, this is the beginning of the Diamond’s end.
Hivi karibuni katika shoo ya Fiesta 2012, Diamond alishindwa kupokea shangwe zilizozoeleka, hata alipoamua kuvua nguo na kubakisha ile ya ndani, bado alichemka. Zaidi akaonekana kuharibu zaidi kuliko kujenga.
Diamond alivua nguo, kipindi ambacho Wema yupo kwenye gumzo zito kutokana na jinsi ambavyo alikuwa anacheza nusu uchi jukwaani katika shoo kadhaa za Fiesta 2012. Kwa maana hiyo, Diamond alipovua nguo ilitafsiriwa amemuiga Wema.
Unapomuiga mtu maana yake unakuwa umemkubali, kwa hiyo Diamond ‘amechizika’ kwa Wema kiasi ambacho hata uchafu anaoufanya yeye anauiga. Kwa mantiki hiyo Diamond na Wema ni kama boyfriend kama girlfriend (like a boyfriend like a girlfriend).
DIAMOND ANAHARIBIKA SI UTANI
Hapati muda wa kufanya mazoezi, anatumia muda mwingi kujiuguza maradhi ya mapenzi. Hii ndiyo sababu kwamba sikushangaa kumuona akichemka jukwaani. Wala sijiulizi ni kwa nini kiwango chake kinaporomoka kwa kasi.
Oktoba 26, 2012 usiku wa kati ya saa 8 na 9, nikiwa naendesha ‘kibebi-woka’ changu nikitokea ofisini kwetu Bamaga, Mwenge, naelekea nyumbani Kijitonyama, nilipofika Mtaa wa Akachube (Kijitonyama), nilimkuta Wema akiwa anaongea na simu huku amezungukwa na watu.
Nikafunga breki, nikashusha kioo nikamsalimia naye akaitika. Nilipoona hayupo kwenye hali ya kawaida nikashuka. Stori niliyoipata pale ni kuwa kumbe alikuwa amegombana na Diamond muda mfupi uliopita.
Eneo la tukio (jirani kabisa na kwa Wema), alikuwepo pia mwanamuziki Omar Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’. Nilipoona mazingira hayavutii, nikamuacha Ommy anamtuliza Wema, mimi nikaondoka zangu.
Asubuhi nikaambiwa kuwa Diamond alirudi nyumbani kwa Wema, suluhu ikapatikana. Jaribu kufikiri kuwa kama mtu usiku wa manane yupo bize na mapenzi, migogoro isiyokwisha ni saa ngapi atatulia kubuni shoo? Ni muda gani atautenga kwa ajili ya kutengeneza staili mpya?
JE, ANAYAJUA YALIYOMKUTA KANUMBA KWA WEMA?
Mungu amlaze mahali pema marehemu Kanumba ambaye ndiye aliyemfanya Wema aingie kwenye ulimwengu wa filamu. Mapenzi yalipokolea, The Great alilewa kiasi kwamba alishindwa kabisa kustahimili vishindo.
No comments:
Post a Comment