Ripoti rasmi ya kifo cha Albert Mangwea, ni ya kiingereza na inapatikana kwenye link ifuatayo: Official medical report on what caused Ngwair’s death. Kwa wale ambao English not richabo, mukhtasari wa ripoti hii kwa Kiswahili ni kama ifuatavyo:
Kwa mujibu wa ripoti hiyo kutoka hospitali alikopelekwa marehemu
Ngwair, Dkt. Shirley Radcliffe amethibitisha kuwa kilichomuua Albert
Mangwair ni sumu ya kilevi. [Ufafanuzi wangu] Kilevi au alkoholi
inayolewesha watu kwenye pombe ni sumu. Ukiinywa kwa kiwango kikubwa,
kinaweza kukusababishia upotevu wa fahamu, kupunguza uwezo wa kupumua,
na hata kifo.
Taarifa hiyo inaendelea kwa kusema kwamba baada ya
kunywa kupita kiasi, Ngwair alitumia mihadarati kwa kiwango kikubwa
kuliko mwili wake unavyoweza kuhimili(drug overdose)iliyoko kwenye
pombe. Dkt Radcliffe aliongeza kuwa Ngwair alipelekwa katika wodi ya
watu mahututi kutokana na upungufu mkubwa wa oksijeni mwilini au
“hypoxemia.”
Mmoja wa rafiki zake alikuta chupa mbili za vodka
zikiwa tupu ndani ya gari, na Ngwair alikua na tatizo la kula linaloitwa
bulimia kwa miezi kadhaa kabla ya kifo chake, ambapo alikua akijirusha
bila kikomo bila kupumzika au kupumzika kidogo.
Sampuli ya
kutoka tumboni kwake inaonyesha mchanganyiko wa kiwango kikubwa cha
mihadarati aina ya cocaine, na heroine, na pia alikutwa akiwa na gramu
0.08 za bhangi kwenye damu.
Kifo chake kilisababishwa na massive
heart attack (shambulizi la moyo?) na kushindwa kupumua,
vilivyosababisha moyo wake usimame na akafariki baada ya sekunde kadhaa
No comments:
Post a Comment