Mwigizaji wa kike
anayetesa katika tasnia ya filamu Bongo Diana Rose kimaro ‘Diana’
amedai kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yoyote na wala
hafikirii kuwa na Boyfriend kwani yeye bado ni mwanafunzi na akili yake
yote ipo katika masomo .
Wakati ukifika akiwa na maisha yake atachagua ni mwanaume yupi anastahili kuwa naye kwa maisha yake rasmi lakini si sasa.
“Sijui
kabisa mambo hayo na sijawahi kufanya upuuzi huo, ninaheshimu sana
familia yangu baba yangu ni mkali sana hataki ujinga. Kwa hiyo si rahisi
kudili na wanaume, mimi ni bikira , natoa nafasi kwa masomo kwanza
sitaki kujichanganya na kuwa kituko mjini,” anasema Diana.
No comments:
Post a Comment