Saturday, September 21, 2013
PICHA NA JINSI TUKIO LA KUVAMIWA SUPER MARKET KENYA
Kwa mujibu wa taarifa za sasa, takriban watu 30 wameripotiwa kuuawa na wengine 60 kujeruhiwa wakati ambapo mapambano ya bunduki yanaendelea kati ya polisi na watu hao wenye silaha walioiteka mall ya Westgate jijini Nairobi, Kenya.
Shuhuda mmoja anadai aliwasikia watu hao wakiwaambia waislam wasimame na kuondokoa na kwamba wasio waislamu pekee ndio waliwalenga.
Balozi wa Uholanzi nchini humo Rob Vandijk ameliambia shirika la AP kuwa alikuwa akipata chakula kwenye mgahawa uliomo ndani ya mall hiyo pindi watu hao wenye silaha waliporusha bomu hilo. Polisi wameizingira mall hiyo na harakati za kuwakomboa watu walioshikiliwa mateka kwenye mall hiyo zinaendelea.
Mall hiyo ni maarufu kwa kuwa na wateja wengi wenye kipato cha juu nchini humo na raia wa kigeni. Polisi imewataka wananchi wakae mbali na eneo hilo kwakuwa bado ni hatari.
Sababu za shambulio hilo hazijafahamika lakini vyombo vya habari nchini humo vinasema kundi hilo laweza kuwa magaidi ama majambazi walioenda kupora.
No comments:
Post a Comment