Hivi majuzi mwanadada Huddah Monroe wa
Kenya alitoa kauli kwenye mtandao kwa mwanamuziki wa kizazi kipya
Diamond platnumz juu ya Wema Sepetu kwa kumwambia kuwa “asihangaike na
wadada wengine kwani wema ndio kipenzi chake na hao wengine wote ni
wapiti njia” kauli ambayo kwa muda mfupi tuu imemfanya mwanadada huyo
awe gumzo la mitandao hapa nchini na “kuchafua hali ya hewa” huko kwenye
mitandao mbalimbali ya kijamii na isiyo ya kijamii kwa watu wanopenda
na wasipoenda penzi la wawili hawa
Uchunguzi uliofanya na bongomovies
umebaini kuwa mashabiki wengi wa muziki na filamu hapa nchini wanapenda
sana mahusiano baina ya wawil hawa (Wema na Diamond) kiasi cha
kusababisha kuanzishwa kwa makundi mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii
yakichochea wawili hawa kuoana na ikiwezekana kuzaa watoto haraka
iwezekanavyo.
Katika pitapita zetu kwenye mtandao
tuliweza kupata kauli hizi za watu mbalimbali wakimsifia Huddah kwa
kauli yake hiyo huku wengine wakimuona kama ni shujaa….
“Umenifurahisha sana leo yaan had nime comment!!@huddahmonroe”
mmoja wapo aliandika…
“Kuanzia leo nakupenda bureee....na nakufollow@huddahmonroe”
mwingine aliongezea…
“Nakupenda bureee Huddah we ni shujaa”…
mwingine naye aliongezea huku wakidiriki kusema kuwa wawili hawa
wakioana basi itakuwa kama siku ya mapumziko ya kitaifa kwao.
No comments:
Post a Comment