Beautiful Onyinye wa Bongo, Wema Sepetu hivi karibuni ameachia picha
tata kwenye akaunti yake ya Mtandao wa Instagram zikimuonesha akiwa
ameacha mgongo wazi, jambo lililotafsiriwa na wengi kuwa ameamua kufunga
mwaka huu kwa staili hiyo ya kuacha mgongo nje,
Katika picha hizo, Wema anaonekana kujichora tatoo kibao kuanzia
shingoni na kumfanya aonekane tofauti na alivyozoeleka jambo lililofanya
wengine wamsifie huku wengine wakimponda mbaya.
“Sasa Wema kujichora hivyo mgongoni ndiyo nini? Bora ungeuacha mgongo
wako kama ulivyokuwa zamani,” alichangia mmoja wa wadau na kuungwa
mkono na wenzake.
Showbiz ilipomvutia ‘waya’ Wema ili kumuuliza kulikoni ameamua kupiga
picha za kuuanika mgongo wake, simu yake ilikuwa ikiita bila
kupokelewa
No comments:
Post a Comment