MSANII nyota wa filamu Bongo
Wema Isack Sepetu amefunguka kwa kudai kuwa hawezi kuvunja urafiki na
meneja wake Martin Kadinda kwa sababu kama kuna kitu chochote cha
mafanikio nyuma yake yupo Kadinda.
Wema Sepetu ameuambia mtandao wa FilamCentral kuwa hana rafiki anayejua siri zake zaidi ya meneja huyo ambaye amekuwa akimuongoza vema.
“Kadinda ndo kila kitu kwangu, hata
akiondoka na kukaa mbali na mimi kwa muda mrefu ninapokutana naye tu,
nitamweleza kila kitu toka siku ya mwisho tuliyoachana, hivyo inakuwa
kama sijapoteana naye,yaani ni kama vile nipo naye kila siku iendayo kwa
Mungu,”anasema Wema.
Msanii huyu ameendelea kusema kwamba hata kampuni yake ya Endless
Fame film aliifungua kwa msaada wa Kadinda baada ya kumshauri kuwa kwa
hadhi yake anastahili kuwa na kampuni na aache kuigiza filamu za watu
wengine.
No comments:
Post a Comment