Tarehe 27.02.2014
majira ya saa 22:15hrs
Huko maeneo ya
Ligula B kata ya Ligula Tarafa ya Shangani Wilaya Mtwara Mkoa Mtwara,ZUWENA MWAPINDI
,Miaka 27,kabila Mnyakyusa,Wakala wa Tigo ,Mkazi wa Ligula B aliuwawa kwa
kuchomwa kisu kifuani kwenye ziwa la upande wa kushoto,Mtuhumiwa ni HABIBU
DASTAN au kwa jina lingine UPSON MILLANZI,Miaka 26,Mkazi wa Dar es salaam,ila
ni mwenyeji Rondo Mitanga,Dereva.Mtuhumiwa alifanikiwa kutoroka mara tu baada
ya kufanya mauaji hayo ila kwa ushirikiano uliopo kati ya jeshi la polisi Mkoa
Mtwara na wananchi mtuhumiwa alikamatwa maeneo ya Namayakata Tarafa ya Ziwani Kata
ya Nanguruwe Wilaya Mtwara Vijijini.Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada
ya upelelezi wa tukio hilo kukamilika.
Rai:Tunapenda
kuwaomba wananchi waendele na moyo huo wa kushirikiana na vyombo vya dora
katika kuwafichua wahalifu katika jamii.
Asanteni
No comments:
Post a Comment