Translate

Saturday, August 25, 2012

AY JUKWAA MOJA NA PAPA WEMBA


Wanamuziki nguli Afrika, wataungana na msanii mahiri wa kizazi kipya nchini Ambwene Yessaya, kutumbuiza wakati wa mechi ya fainali ya michuano ya Airtel Rising Stars, itakayopigwa leo Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Nyota watakaotumbuiza katika fainali hiyo ni Papa Wemba wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), 2 Face Idibia wa Nigeria, Ambwene Yessaya na Daddy Owen wa Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na waandaaji wa michuano hiyo, wanamuziki hao wataanza kutoa burudani kuanzia mchana ambapo kila mmoja atatumbuiza nyimbo zilizompatia umaarufu ndani na nje ya nchi yake.

Baadhi ya nyimbo hizo ni ‘African Queen’ na ‘If love is a crime’ za 2 Face Idibia, ‘Show me the way’ ya Papa Wemba na ‘Bed n Breakfast‘, ‘Goodlook’ na ‘Freeze’ za Ay.

No comments: