Mwanamuziki
mkongwe katika Taarab Fatuma Bint Mbaraka maarufu kwa jina la Bi
Kidude amefariki dunia muda mchache uliopita huko Bububu Zanzibar,
sehemu alikokuwa anaugulia kwa kipindi sasa. Mwili wake utahamishiwa
kwake Rahaleo na mazishi yatakuwa kesho. Bi Kidude alizaliwa katika
kijiji cha Mfagimaringo, alikuwa binti wa mchuuzi wa nazi, hakuna
anayejua haswa Bibi huyu alizaliwa tarehe ngapi, kuna hata mawazo kuwa
alikwishafikisha miaka 102. Katika mwaka 1920 tayari alikuwa
amekwisha anza kuimba katika vikundi vya sanaa kule kwao, mwaka 1930
alijiunga na Egyptian Musical Club ya Dar es Salaam na kuzunguka miji
mingi ya Tanganyika wakati ule , mwaka 1940 alirudi Zanzibar ambako
awali alikuwa amekimbia kwa kuwa aliozwa kwa nguvu na mtu aliyemzidi
sana umri. Bi Kidude pia liwahi kuimba na Sitti Binti Sadi wakati wa
ujana wake, na katika maisha yake Bi Kidude amekwisha zunguka mabara
yote akiimba katika majukwaa na wanamuziki maarufu ulimwenguni Mungu Amlaze Pema Peponi Bibi yetu. Amen
No comments:
Post a Comment