Translate

Tuesday, May 7, 2013

JWTZ WASHATUA CONGO-M23 WANAPIGA KAMPENI KUWAJENGA CHUKI KWA WANANCHI


Kwa mujibu wa muandishi alie na wasi hao Diana Katabarwa kwenye Blog yake ya congo DRC NEWS anamnukuu kiongozi wa kisiasa wa M23 Mr. Bisimwa akiwambia wakaazi wa North Kivu kuwa majeshi ya Tanzania na South Africa nimajeshi dhalimu yaliyo jaa rushwa na hayawezi kuibadili Congo ila yamekuja kuiba mali na kumsaidia KABILA awatawale huku jeshi lake la FDLR na waasi wa MAI MAI watapewa na fasi ya kuwa pora mali zao na kuwabaka wake zao na watoto.

Pia bwana Busimwa anadai kinyume na taarifa zilivyo kikosi cha jeshi la Tanzania kikiwa na askari 450 kimesha ingia mashariki ya CONGO kwenye mji wa UVIRA SOUTH KIVU huku Kamanda wao (TPDF) akiwa mjini Goma. kikosi cha jeshila SOUTH AFRICA kiko mita 20 kutoka waasi walipo kwenye mji wa MUNGI nje kidogo ya GOMA. Pia aliwaeleza wananchi hao kuwa kuna makomandoo 30 wa jeshi la Ufaransa ambao wako mjini GOMA wamefikia Linda Hotel, BUSIMWA alidai wafaransa ndio walisimamia mauaji ya kimbari ya rwanda kwahiyo kuwepo kwao ni ishara mbaya kwa wakazi wa mashariki ya CONGO ambao wengi ni watusi.

kila laheri TPDF.

No comments: