WANAUME WAWILI WAFUMANIWA WAKILAWITIANA KWENYE NYUMBA YA WAGENI
MWANAUME aliyefahamika kwa jina la baba Salome, mkazi wa Tandika jijini Dar es Salaam, hivi karibuni alimdhalilisha mkewe (mama Salome) baada ya kufumaniwa gesti akiwa na mwanaume mwenzake ambapo madai yalisema, walikuwa katika hatua za mwisho za kuingiliana kimwili…
Aibu hiyo ya mwaka ambayo ilionekana pia kama kituko ilijiri Mei 3, mwaka huu ndani ya gesti moja maarufu iliyopo Devi’s Corner –Tandika, jijini Dar es Salaam.
Awali ilidaiwa kuwa, mwanaume huyo na baba Salome mwenye mke na watoto wawili wanaomtegemea kwa kila kitu, walionekana wakiingia kwenye gesti moja ambayo pia ipo maeneo hayo hali iliyozua maswali kwa watu waliokuwa wakiwafahamu.
“Unajua tatizo lilianzia wapi? Baba Salome na yule mwanaume
mwenzake walionekana wakiingia gesti moja kisha wakatoka, wakaingia
nyingine pia wakatoka, ndipo watu wanaowafahamu wakajiuliza kulikoni
wawili hao kutembelea gesti siku hiyo, wakawafuatilia,” alisema mnyetishaji mmoja.
Akaendelea: Lakini watu waliwafahamu kwa namna mbili tofauti, baba
Salome ni mtulivu, mwadilifu, mwenzake watu wanasema ana ‘katabia’ ka
kutaka kuwa faragha na wanaume wenzake bila kujulikana nini anakitaka
katika usiri huo.
Madai zaidi yakawekwa wazi kwamba, baadhi ya watu walikwenda
kwenye gesti walizokwenda wawili hao na kuulizia nini walikuwa
wanakitaka, ndipo siri ikawekwa wazi kwamba wanatafuta chumba cha
kupumzika kwa siku hiyo lakini kwa sheria za Jiji la Dar es Salaam (kama
siyo za nchi nzima), wanaume wawili hawaruhusiwi kulala chumba kimoja.
Chanzo kikasema: Wambeya wakawaona wakiingia kwenye gesti ya
tukio, wakapewa chumba. Ndipo wakakimbia nyumbani kwa baba Salome na
kumtonya mkewe, mama Salome kwamba mumewe ameingia gesti.
Kichekesho zaidi kinaangushwa kwamba, baada ya kuambiwa mumewe amezama
gesti, mama Salome ambaye ndiyo kwanza alikuwa amefika kutoka kwenye
mikopo ya Finca, alitoka mbio huku akisema anakwenda kumtoa sikio la
kulia Kidawa akiamini mumewe ameingia gesti na mwanamke huyo. “Watu
walimwambia mumewe hakuingia gesti na Kidawa bali mwanaume mwenzake.
Kwanza mama Salome aliomba asitaniwe juu ya hilo, lakini
akasisitiziwa,” alisema mtoa habari huyo.
Akizungumza kwa jazba na waandishi wetu nje ya gesti hiyo, mama
Salome alisema kwamba alipata taarifa siku nyingi mumewe ana ukaribu na
mwanaume huyo ambaye mitaani watu wanasema anajihusisha na vitendo vya
ushoga.
“Nilipozipata taarifa hizi sikuziamini, nilidhani ni Kidawa ndiyo kaingia gesti na mume wangu, maana Kidawa ndiye mbaya wangu,” alisema mwanamke huyo kisha akazama ndani ya gesti akiwa na polisi ambao haikujulikana walikotokea.
Huku mumewe na mwanaume mwenzake wakiwa hawana hili wala lile kule
chumbani, mlango ulisukumwa na kufunguka ambapo mwanamke huyo aliwakuta
wawili hao wakiwa wameshavua baadhi ya nguo.
Wote walishtuka kuona wameingiliwa! “Yaani roho inauma sana, sijui ni kitu gani umekosa kwangu mpaka unakuja kwa mwanaume mwenzako jamani baba Salome,” alisema huku akilia mama Salome.
Baada ya kugundua wamenaswa, mwanamke aliyekuwa na baba Salome
aliangua kilio huku akiomba kusamehewa kwa vile yeye ni mume wa mtu,
lakini kilio chake hakikusikika kwa polisi ambapo waliwafunga pingu na
kuwataka kuelekea katika kituo cha polisi.
Wakati wakitoa maelezo kwenye kituo cha polisi, mwanaume aliyekuwa
na baba Salome alijitambulisha kwa jina la Julius Mwita, mkazi wa
Devi’s Corner ana mke na watoto wawili na aliwaomba sana waandishi
wamhifadhi kwani wakwe zake wakimuona ‘itakula kwake’.
“Jamani nipo tayari kwa lolote naomba sana tuyamalize hapahapa,
mimi ni mume wa mtu, wakwe zangu wananiheshimu na kunithamini sana,” alisema Mwita
Hata hivyo, pamoja na kilio hicho mwanaume huyo aliishia kuswekwa
lupango na baadaye kuhamishiwa katika Kituo cha Polisi cha Chang’ombe
kwa hatua zaidi.
No comments:
Post a Comment