ALIYEPIGWA SHOKA KICHWANI NA MAJAMBAZI AFARIKI DUNIA
Wadau
picha hizi zinatisha lakini mtuwie radhi kwani ndiyo hali halisi
iliyotokea usiku wa kuamkia leo huko Tabata na hakuna mtu anayeweza
kuvumilia maovu haya yanaofanywa na watu wasiokuwa na utu. Leo saa 12
asubuhi hospitali ya taifa Muhimbili imempokea mgonjwa anayeitwa Mussa
Shabani(42) akiwa na shoka iliyonasa kichwani
(kama picha inavyooneka hapo juu ).
Bwana
Mussa ni mlinzi katika nyumba ya Joseph Mwakyusa huko Tabata. Majambazi
yalipofika nyumbani kwa bawanaMwakyusa yalimjeruhi kwa shoka bwana
mussa na, wakati majambazi yaliyovamia nyumba ya Mwakyusa yakiendelea
kufungua spea za gari aina ya Toyota verosa. kwa bahati nzuri bwana
Mwakyusa alishtukana ndipomajambazi hayo yalipokimbia na kutoweka
yakimuacha mussa katika hali mbaya na shoka ikiwa imenasa kichwani.
Madaktari wa taasisi ya tiba ya mifupa MOI walifanya kazi ya ziada kuitoa shoka hiyo na sasa Mussa yupo chumba cha wagonjwa
mahututi. bwana.
Jumaa
Almasi afisa uhusiano mkuu wa MOI amethibitisha tukio hilo na kusema
''Ni kweli bwana Mussa amepokelewa hapa MOI akiwa na shoka iliyonasia
kichwani mwake lakini madaktari wamemfanyia upasuaji na kuitoa na sasa
hivi yupo chumba cha wagonjwa mahututi''
No comments:
Post a Comment