Translate

Friday, February 28, 2014

TUKIO LA MAUAJI-HUKO MKOANI MTWARA






Tarehe 27.02.2014 majira ya saa 22:15hrs
Huko maeneo ya Ligula B kata ya Ligula Tarafa ya Shangani Wilaya Mtwara Mkoa Mtwara,ZUWENA MWAPINDI ,Miaka 27,kabila Mnyakyusa,Wakala wa Tigo ,Mkazi wa Ligula B aliuwawa kwa kuchomwa kisu kifuani kwenye ziwa la upande wa kushoto,Mtuhumiwa ni HABIBU DASTAN au kwa jina lingine UPSON MILLANZI,Miaka 26,Mkazi wa Dar es salaam,ila ni mwenyeji Rondo Mitanga,Dereva.Mtuhumiwa alifanikiwa kutoroka mara tu baada ya kufanya mauaji hayo ila kwa ushirikiano uliopo kati ya jeshi la polisi Mkoa Mtwara na wananchi mtuhumiwa alikamatwa maeneo ya Namayakata Tarafa ya Ziwani Kata ya Nanguruwe Wilaya Mtwara Vijijini.Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi wa tukio hilo kukamilika.
Rai:Tunapenda kuwaomba wananchi waendele na moyo huo wa kushirikiana na vyombo vya dora katika kuwafichua wahalifu katika jamii.

 Asanteni

No comments: