Sunday, March 25, 2012

WACHEZAJI WA YANGA WALIOFUNGIWA WAACHIWA HURU

Kamati ya Nidhamu ya TFF - imewachia huru wachezji watano (5) wa klabu ya Yanga waliokuwa wamefungiwa kutokucheza mpira kwa vipindi tofauti na kamati ya ligi ya TFF, baada ya kamati ya nidhamu kuridhika na maelezo ya utetezi wa klabu ya yanga juu ya adhabu hizo zilizotolewa wiki mbili zilizopita.
Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu - TFF Mh.Afred Tibaigana alisema kwa mujibu wa taratibu za shirikisho la mpira wa miguu nchini - TFF kamati ya ligi haina mamlaka ya kumfungia mchezaji yoyote wala kutoa adhabu kwa mchezaji yoyote isipokuwa kamati ya nidhamu ndo yenye mamlaka hayo.
Tibaigana alisema kamati ya nidhamu ndo yenye wajibu wa kuwawajibisha wachezaji na viongozi wanaopatikana na hatia katika mpira wa miguu, hivyo maamuzi yaliyofanywa na kamati ya ligi sio halali, hivyo kama bado wanataka kuwashitaki tena wachezaji hao inabid wapeleke malalamiko yao upya kwa kamati ya Nidhamu.
Awali kamati ya ligi ya mashindano iliyokutana tarehe 12.03.2012 chini ya mwenyekiti wake Godfrey Nyange Kaburu ilitoa adhabu kwa wachezaji watano (5) wa yanga kutokana na kile walichokiita utovu wa nidhamu kwa wachezaji wa yanga katika mchezo dhidi ya Azam fc, mchezo uliochezwa machi 10 mwaka huu.
Kamati hiyo ya ligi ilitoa adhabu ya kumfungia mchezaji Stephano Mwasika mwaka mmoja kutocheza mpira na faini ya tsh milioni moja.
Jeryson Tegete alifungiwa kutocheza ligi kuu kwa miezi sita (6) na faini ya sh.500,000.
Nadir Haroub Cannavaro alifungiwa kutocheza ligi kuu kwa mechi sita (6) na faini ya sh.500,000.
Nurdin Bakari alifungiwa kutocheza mechi tatu (3 )za ligi kuu na faini ya sh.500,000.
Omega Seme alifungiwa kutocheza mechi tatu (3) za ligi kuu na faini ya sh.500,000.
Kutokana na maamuzi ya kamati ya nidhamu - TFF wachezaji hawa watano (5) waliokuwa wamefungiwa kwa sasa wapo huru na wanaruhusiwa kucheza michezo inayofuata katika ligi kuu mpaka hapo TFF itakapopeleka malalamiko mapya juu ya wachezaji hao kwa kamati ya nidhamu.
Klabu ya Yanga itawatumia wachezaji wake hao katika mchezo dhidi ya timu ya Coastal Union ya tanga jumamosi ijayo katika mchezo wa ligi kuu utakaofanyika jijini tanga machi 31-2012
Katika hatua nyingine kesi iliyokuwa inawakabili Louis Sendeu Afisa Habari wa klabu ya Yanga na Ismail Aden Rege mwenyekiti wa klabu ya Simba, juu ya kutishia kutopeleka timu uwanjani katika mchezo wa Ngao wa Hisani ulofanyika august mwaka 2011, kamati hiyo ya Nidhamu imewapa onyo kutorudia kitendo hicho, kwani kufanya vile ni kuchochea uvunjani wa amani katika michezo.

No comments:

Post a Comment