HII NDIO KAULI YA ERICK SHIGONGO KUHUSU CHAMELEON
MD wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo, mapema jana ameongea na media kuhusu madai ya Jose Chameleone kudai paspoti yake, ambaye juzi alikwenda Ubalozi wa Tanzania nchini kwao akiwa na washabiki wake na mabango kushinikiza kurejeshewa paspoti yake.
Eric amefunguka kwa kusema kuwa, kampuni yake na msanii huyo waliingia makubaliano ya kufanya shoo kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini, liliofanyika Uwanja wa Taifa Julai 7 mwaka huu, ambapo katika mazungumzo ya awali, msanii huyo aliomba kulipwa dola 5000 na kulipiwa tiketi 2 za ndege ili kuhudhuria tamasha hilo, masharti ambayo yalikubaliwa.
Mazungumzo hayo ya awali yalifanyika kati ya Global Publishers na agent wa Chameleone ajuliikanae kwa jina la George. Kabla ya kutuma fedha hizo, kampuni yake ilihitaji kujiridhisha kama agent huyo alikuwa kweli anawasilina na kukubaliana na Chameleone kuhusu shoo ya Dar, ili kuepuka utapeli.
“Tulipokubaliana nae kupitia agent wake, tuliamua kwenda mbele zaidi ili kujiridhisha, ambapo tuliwasiliana na mwanamuziki Kidumu ambaye anamfahamu huyo George na kwenda mpaka Kampala kukutana ana kwa ana na wahusika, kwa niaba yetu”, alisema Shigongo.
Akielezea zaidi, Shigongo alisema kuwa Kidumu alikwenda Kampala na kukutana na George pamoja na Jose Chameleone, ambaye alikubali kuja kufanya shoo na kumruhusu Kidumu kusainishana mkataba na ajenti wake na kumpatia hizo fedha.
“Chameleone alitoa ruhusa kwa agent wake kusaini mkataba na kupokea advance ya dola 3,500 kwa niaba yake kwa madai kuwa yeye asingeweza kusubiri malipo wakati huo kwa sababu alikuwa anawahi sehemu nyingine.
“Baadae Jose alikuja kugeuka na kudai hakupewa hizo pesa na agent wake, kitu ambacho kilonekana kama mchezo wa kitapeli kati ya Chameleone na agent wake kwetu sisi.
“Kwa kuwa ujio wake Tanzania ulikuwa umeshatangazwa sana, uongozi wa Global Publishers, ulilazimika kufanya mazungumzo mengine na Chameleone na kumuomba sana kuja nchini kufanya shoo, ambapo this time akakubali kwa masharti ya kulipwa dola 8000 na tiketi nne za ndege.
“Ndugu zangu, sikuwa na jinsi, nililazimika kumkubalia na kumlipa dola 8000, kwa sababu tayari tamasha lilikuwa limeshatangazwa sana, billboards zimewekwa barabarani na promosheni kubwa ilikuwa inafanyika,” alisema Shigongo kwa uchungu.
Hivyo mara baada ya kukubaliana, safari hii akalazimika kumtuma meneja wake kwenda mpaka Kampala na kukutana na Chameleone ana kwa ana na kumpatia dola 8000 na kusaini mkataba mwingine wa pili.
“Ni dhahairi kabisa alichokifanya Chameleone kilikuwa ni utapeli kwa kushirikiana na agent wake, kwa sababu tunamuamini Kidumu ambaye tumeshafanya naye kazi mara Kadhaa kwa uaminifu mkubwa. Pia ni Chameleone ndiye aliyemuidhinisha agent wake kuchukua pesa hizo, hivyo ulikuwa ni mchezo wa pamoja, na hiyo ni tabia ya Chameleone, kwani ameshawafanyia mapromota wengi kiasi kwamba hivi sasa hakanyagi nchini Kenya.
“Dola 3,500 siyo fedha nyingi, ningeweza kuzisamehe, lakini nimeamua kuzidai kwa manufaa ya watu wengine, Watanzania tusikubali kufanywa wajinga kwa sababu ya upole wetu, tutaendelea kudhauriwa na kufanywa wajinga mpaka lini,” alihoji Shigongo.
Mwisho Shigongo alitoa wito kwa Watanzania kuungana katika suala hili, kwani Chameleone ameonesha dharau kubwa kwa Watanzania kwa kumfuata balozi wetu nchini Uganda na kuondoka ofisi kwake huku akisonya na kubamiza mlango, akiendelea kuonesha dharau kwa Watanzania wote wapatao miloni 40!
No comments:
Post a Comment