Sunday, July 29, 2012
TUNAELEKEA WAPI WASANII WA TANZANIA?
Stori Waandishi Wetu
MLIMBWENDE mtata Bongo, Jacqueline Patrick, kama kawa, amedondosha picha nyingine chafu kwenye ‘peji’ yake ya mtandao wa BBM, Risasi Jumamosi lina ‘fulu’ data.
Jack ambaye ni mke wa mfanyabiashara Abdulatif Fundikira alitupia picha hizo Julai 25, mwaka huu huku akizisindikizia na ujumbe usemao ‘sina tatizo na mtu na mwenye macho haambiwi tazama.’
Picha hizo zimezua maswali mengi kwa watu wake wa karibu ambao wengi ni waumini wa dini ya kisilam ambao kwa mwezi huu wapo ndani ya swaumu.
Wengi walihoji nini kilimfanya staa huyo kuweka picha hizo chafu sana zenye kumwonesha kila kitu huku akiwa ameolewa kwa ndoa! “Au yuko sokoni zaidi?” alihoji mdau wake mmoja.
Jack bila kujali hilo aliendelea kuanika picha hizo kwa kubadilisha moja baada ya nyingine kulingana na mapozi aliyotaka mwenyewe.
Mara kwa mara Jack amekuwa akipiga picha zenye kuonesha asilimia 95 ya umbile lake bila nguo na kuzitupia kwenye mitandao.
No comments:
Post a Comment