KAMATA KAMATA YA WEZI WA KAZI ZA WASANII WA FILAM IKIENDELEA
Wasanii na wadau wengine waingia Mtaani na kukamata Dvd Feki kibao Maharamia wapatikana jirani kabisa na Maduka yanayouza kazi halali, Naibu Waziri Makala asikitishwa na wizi huo wa kazi za wasanii hapa nchini .. wimbi la wizi wa kazi za wasanii wa filamu limeshamili zaidi na kukua kila kukicha Kampuni ya Steps Entertainment kwa kushirikiana na wadau wa filamu kuendesha msako kwa maharamia wanaojinufaisha kwa kazi za wasanii bila idhini ya wenye mali, mwizi wa kwanza alikamatwa siku ya Jumanne asubuhi baada ya mtego uliowekwa kumnasa Haramia mkubwa maeneo ya Kariakoo.asubuhi katika maeneo ya mtaa wa Magila na Likoma HaramiaBaadi ya wasanii walisikika wakisema “Hawajui shida tunazopata huko location kila siku tunagombana na
wasambazaji wakidai filamu zetu haziuzi lakini mtaani tunaziona kwa wingi, tunaumiza vichwa kumbe mwizi mwenyewe yupo jirani hata hatua kumi hazifiki, ninaumia sana maisha ninayoishi kwa kufanya kazi ngumu kisha kuna wanyonyaji wanakula bila kutoka jasho, watu kama hawa ni kuwafunga maisha,”Aidha nae Rais wa Shirikisho la filamu ameeleza kuwa kampeni za kamatakama zimeanza baada ya kupewa idhini na Mh. Amos Makala Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Michezo na Vijana
No comments:
Post a Comment