Tuesday, September 4, 2012
BEN POL :ASEMA HAITAJI KUSHIRIKISHWA KWA SASA
Kwa sasa msanii huyo anatamba na singo yake ya 'Maneno Maneno', alisema kwamba kufanya kazi za wengine kunamfanya achelewe kumamilisha mipango yake.
Si mwingine bali ni yule Msanii wa miondoko ya R&B nchini , Ben Pol, alisema kwamba hawezi kushiriki kufanya kazi za wasanii wengine ‘Collabo’ mpaka atakapokamilisha matayarisho ya albamu yake inayokwenda kwa jina la Pete.
Pol alisema kwmaba kitendo cha kujikita kwenye kazi za wasanii wengine, kinachukuwa muda wake mwingi na matokeo yake wenzake hukamilisha albamu zao huku za kwake zinalala.
“Hii ndiyo sababu ya kutoshiriki katika kazi ya msanii yeyote kwa sasa, mtaniwia radhi kwa wale ambao nitakwaza kwa uamuzi huu…tuvumiliane nitakapomaliza nitashiriki tu,” alisema Pol.
Mbali na hayo mipini ya msanii huyo kwa sasa ni pamoja na Nikikupata, Samboira, Pete na Yatakwisha aliomshirikisha Linah na nyinginezo.
No comments:
Post a Comment