Mkali wa Bongo fleva, Emmanuel simwinga Izzo B, ametanuka kisanii na sasa ametupa kete yake nyingine kwenye filamu ya My Princess aliyocheza na mrembo mwenye mvuto wa kipekee Jacqu
eline Wolper Massawe.
Izzo B alisema yeye ni msanii mwenye vipaji vingi na huu ni wakati wake kuonesha watanzania kuwa hata kuigiza yupo poa.
"Huu ni mwanzo tu, baada ya hii nitakuja na vitu vikali zaidi. Natamani sana mashabiki wangu waone kazi niliyoifanya, najua watanikubali tu. Sijabahatisha niko vizuri ndiyo maana nimeona nijaribu na upande wa pili kama wanavyofanya wasanii wa mamtoni" Alisema Izzo B.
No comments:
Post a Comment