Wednesday, November 7, 2012
RAIS OBAMA KAINGIA IKULU TENA KWA MIAKA MINNE !!
ALIYEKUWA mgombea wa urais wa Marekani kupitia chama cha Democratic, Barack Obama, amemshinda mpinzani wake kutoka chama cha Republican, Mitt Romney, katika uchaguzi uliofanyika jana.
Obama ambaye alishinda urais wa nchi hiyo miaka minne iliyopita, amesema hivi sasa ana dhamira ya hali ya juu zaidi na nguvu zaidi za kufanya kazi zake. Aliyasema hayo huko Chicago wakati wa hotuba yake ya kupokea ushindi huo.
Hata hivyo, wagombea wote wawili wa kinyang’anyiro hicho walitoa wito wa umoja kwa watu wa nchi hiyo kwa ajili ya maendeleo.
Katika hotuba hiyo alimshukuru mkewe na mabinti zake , Sasha na Malia, ambao alisema ni “wasichana wawili jasiri kama mama yao.”
Katika uchaguzi huo Obama alipata kura nyingi hususani katika majimbo ya Ohio, Iowa, Wisconsin, Pennsylvania, New Hampshire na Virginia.
Kiongozi huyo alipongezwa haraka na viongozi wengine duniani wakiwemo David Cameron wa Uingereza na Benjamin Netanyahu.
No comments:
Post a Comment