Wednesday, November 7, 2012
WEMA: MAMA USIJE KWANGU HADI…
KITENDO cha staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu kuwaambia walinzi wake kuwa kama hajatoa maagizo yoyote kwamba mama yake, Mariam Sepetu anakuja, akifika mlangoni asifunguliwe kimewashangaza wengi.
Awali, Wema alieleza kuwa, ameweka utaratibu wa watu kuonana naye na kwamba wale watakaokwenda kwake bila taarifa watakuwa wanaishia getini.
Maelezo hayo yalimfanya mwandishi wetu amuulize kama hata mama yake akienda kwake bila ‘apointimenti’ hawezi kuingia ndani ambapo alisisitiza kwa kusema kuwa, utaratibu huo ni kwa watu wote akiwemo mzazi wake huyo.
“Akija bila taarifa hawezi kuingia ndani. Si yeye tu, hata dada yangu, rafiki yangu yoyote yule, meneja wangu hata wewe kama sijatoa maagizo kwa walinzi basi ujue utaishia nje na ukinipigia simu huwa sipokei,” alisema Wema.
Kauli hiyo iliwafanya baadhi ya watu kumshangaa kwa kusema kuwa, utaratibu huo si mzuri kwani kufikia hatua ya kumtaka hadi mama yake aweke ‘apointimenti’ ndipo amtembelee ni kutafuta laana.
“Huyu anatafuta laana, yaani mama yake asiende kwake hadi aweke ‘apointimenti’? Yaani kweli mama yake anaweza kufika getini na asifunguliwe eti kwa kuwa ameenda bila taarifa! Hao wanaomshauri wanampotosha,” alisema Josephine wa Kinondoni.
No comments:
Post a Comment