JAQLINE WOLPER AFUNGUKA !! MAPENZI YA KWELI NDIO MPANGO MZIMA PESA BAADAE
Nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood Jaqueline Wolper ‘Wolper
Gambe’ amedai kuwa hawapendi sana wanaume wenye fedha kwani wengi wao ni
waume za watu, kwa hiyo kwa kuwa nao si rahisi kuonyesha mapenzi yao ya
dhati kwake kwani mapenzi yao ni chumbani tu, lakini hawezi kutembea
nao hadharani kwa kuhofia ndoa zao.Unajua unapokuwa na mtu mwenye fedha
zake alafu mtu mzima hivi unakosa penzi la kweli kwani mapenzi yenu ni
chumbani tu, hamuwezi kutembea pamoja kukaa kama vile ni wapenzi lakini
ukiwa na kijana ambaye ni rafiki hana pesa na wewe una kazi lazima
akuonyesha jinsi mapenzi yalivyo kwa kukuweka karibu kimahaba na wewe
ukafaidi penzi kutoka kwake”,
“Wengi watu wenye pesa zao kuna wakati wananiona nina dharau lakini mimi
ni binadamu nahitaji haki yangu kama mwanamke ya mtu anayenijali na
kuwa karibu na mimi sasa kuna watu wanaamini pesa zao ndio kila kitu,
kiukweli kwangu siyo hivyo ukileta mapenzi hayo lazima unione nina
dharau”,anasema Wolper Gambe.
Aidha kuna watu ambao uwanyooshea vidole wasanii maarufu kama yeye kwa
kuwaona kama vile ni Malaya lakini wanasahau kama nao ni binadamu na
wanaroho kama wanadamu wengine wao si malaika wanapenda na kupendwa, kwa
hiyo ukimuona ana kijana Serengeti boy ujue ni kwa ajili ya kupata
penzi nzito na kusikilizwa haja zake.
No comments:
Post a Comment