Mwigizaji Irene Uwoya ambae alipata tuzo
ya Steps kama mwigizaji bora kike 2012/2013 amethibitisha kuacha
kuigiza movie kwa sasa ili kufanya kazi ambayo ameianza hivi karibuni.
Namkariri akisema: “Nimeamua kuacha
mambo ya movie na kuwaachia wengine, haya maamuzi nimeyafanya kama miezi
sita iliyopita… Mara ya mwisho kuigiza ni zaidi ya miezi sita iliyopita
pia.”
Irene ambae ni mama wa mtoto mmoja kwa
sasa anafanya show ya TV ya kusaidia Watanzania wanaoishi kwenye nyumba
ambazo ni mbovu au hazina mahitaji muhimu yanayotakiwa kwenye nyumba.
Ni show ambayo haitahusika kujenga
nyumba bali kuzirekebisha kwa gharama za mamilioni kwa kutegemea ubovu
wa nyumba yenyewe, ambapo Irene amethibitisha hakuna kiwango cha mwisho
cha pesa kama bajeti ya kutengeneza nyumba moja bali lengo ni kukarabati
nyumba ikamilike.
Movie alizocheza mpaka sasa zinafika 40
lakini za kwake ni nne tu na amekiri kwamba kuacha kwake kuigiza hakuta
mshushia kipato chake cha siku zote ambapo kwa movie moja ya kwake
mwenyewe alikua anaiuza mpaka kwa milioni 35.
Show yake ya TV imeshaanza kuonekana
Tanzania pamoja na kupata wadhamini ambao watamuwezesha kwenye kazi hii
kubwa ya kupokea maombi ya Watanzania mbalimbali ambao wanahitaji nyumba
zao zirekebishwe bure, kupitia kipindi hicho cha TV.
No comments:
Post a Comment