Msanii wa filamu bongo,na
mwenye jina kubwa kuliko umri wake,Elizabeth Michael aka LULU,
ameonesha msimamo mkali baada ya msanii wa bongo fleva mwenye jina la
madini expensive Naseeb Mohamed au DIAMOND kufanya kila aina ya mbinu
ikiwemo ile ya kutaka kumuagizia msanii huyo gari expensive aina ya
nissan murrano yenye thamani ya shiling million zaidi ya 60,ambapo hata
hivyo mbinu yake iyo imeonekana kugonga mwamba baaada ya Lulu kukataa
kata kata kutoka na staa huyo anayetamba na ngoma ya my number one.
Kwa kumaanisha kuwa hataki kutoka na
staa huyo, Lulu alilazimika kubadilisha namba ya simu yake ya mkononi
ili kuepuka usumbufu kutoka kwa bwana mdogo huyo ambaye kila kukicha
amekuwa akiwindwa na wasichana warembo ili tu waonje sukari yake.
Pia inasemekana lengo la diamond
kutaka kutoka na Lulu ni kutaka kukuza jina lake(kiki) kwa kuwa
anaamini staa huyo ana jina kubwa na lenye mvuto hivyo kumfanya na yeye
aogelee kwenye dimbwi la umaarufu na kuongelewa zaidi na watu,na kuwa
ishu iyo ndo itakuwa habari ya mujini yaan yeye kutoka na lulu.
Baadhi ya watu wameonyesha kushangzwa
sana na msimamo mkali wa binti huyo,kwa kuwa waliamini hakuna staa
yeyote bongo mwenye ubavu wa kupindua kwa diamond,kama ilivyokuwa kwa
Wema,Jokate,Aunt,Wolper na baadhi ya mastaa ambao dogo huyo aliwamega
kiulaini.
Watu wanahaha kumjua mwanaume anayempa jeuri Lulu hadi kufikia hatua ya kuchomoa kwa diamond..
No comments:
Post a Comment