MOYO huhifadhi mengi mazito hasa ya
kuumiza! Staa mkubwa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe
amejikuta akimwaga machozi wakati akianika siri tano nzito kuhusu
mapenzi katika mahojiano (exclusive interview) na Amani kwa takriban saa
mbili.
Katika ‘intavyu’ hiyo iliyofanyika Jumatatu iliyopita kwenye Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar kuanzia saa 8:44 alasiri hadi saa 10:44 jioni, Wolper alifunguka vitu vingi.
KISA/MKASA
Akizungumza kwa masikitiko, uchungu na majuto, Wolper alisema hawezi kumsahau mwanaume huyo ambaye ni Abdallah Mtoro ‘Dallas’ kwa namna alivyomwingia kijanja na kutaka kumvunjia heshima aliyoijenga karibia miaka kumi nyuma.
ALIANZIA WAPI NA DALLAS?
“Siku ya kwanza Dallas alinipigia simu
na kuniambia aliniona Magomeni (Dar). Naikumbuka sana siku hiyo, ilikuwa
baada ya mizunguko yangu, mwanzoni sikupokea simu yake kwa sababu
ilikuwa namba ngeni kwangu.
“Nilimsikiliza sana. Jamani yule
mwanaume anaongea kwa ushawishi wa hali ya juu mno. Nilishangaa
aliponieleza kila kitu kuhusu familia yangu na nyumbani kwetu. Kumbe
tayari alishaunda urafiki na baba yangu (mzee Massawe).
“Mwanzoni nilidhani ni tapeli.
Nikamkatia simu. Akaendelea kunipigia na nilipoona imekuwa kero kubwa
nilipokea. Ili kuthibitisha anawajua wazazi wangu, alinitajia namba zao
za simu ambazo ni za kweli.
“Pamoja na hilo nilimfanyia nyodo, si unajua mtoto wa kike? Lakini aliniongelesha kwa upole hadi nikapunguza nyodo zangu.
“Aliniuliza nataka anifungulie biashara
gani. Nikamwambia biashara ya nguo. Akaniuliza nataka mtaji kiasi gani.
nikamwambia dola laki moja kwa sababu nilikuwa sitaki fremu moja,
nilitaka nyumba nzima. Akaniambia hakuna tatizo.
“Pia aliniuliza naishi wapi? Nikamwambia Sinza (Dar) alionesha dharau kwenye simu akaniambia atanihamishia Mbezi Beach.
“Aliniuliza natembelea gari gani? Nikamwambia Toyota Noah. Akaniambia ningependa aninunulie gari gani? Nikamjibu Toyota Discovery lakini yeye akasema ataninunulia Toyota Harrier.
“Kweli baada ya siku mbili-tatu
nililetewa Toyota Harrier nyeusi nyumbani. Niliogopa isijekuwa mtego
nikaingia kwenye matatizo hivyo nilimzungusha mtu aliyeniletea hadi
Sinza-Mori nikamwambia apaki kwenye kituo cha teksi, nikaenda na dereva
nikalichukua hadharani ili lolote likitokea nipate msaada.
“Nilikabidhiwa funguo za lile gari na
documents zake, nikaondoka nalo hadi nyumbani kwangu. Kesho yake Dallas
alimtuma mtu aniletee dola za Kimarekani 15,000 (zaidi ya Sh. milioni 24). Nilipouliza za nini aliniambia ni kwa ajili ya shopping ya kutembelea Harrier niachane na zile swaga za kwenye Noah (fedha inaongea). Kisha akanitumia cheni ya dhahabu.
“Siku iliyofuata alinitumia Sh. milioni
15 nipeleke nyumbani nikawaambie wazazi nimepata mchumba ambaye angeenda
kujitambulisha baadaye. Niliwaambia ni Dallas ambaye walikiri kumfahamu
kwa sababu alishawapigia simu na kujitambulisha kuwa ni mkwe wao.”
AMESHAKUTANA NA DALLAS?
“Hadi hapo nilikuwa sijamuona Dallas kwa sura na fedha nilikuwa natumiwa kila siku.
“Wakati hayo yakiendelea akaagiza nihamishiwe Mbezi Beach na kununuliwa lile gari lililoibua mzozo BMW X6.
“Nakumbuka siku niliyokabidhiwa lile
gari nililia sana. Sikuamini macho yangu kwa sababu Dallas aliniambia
amenitumia kazawadi kumbe ni BMW X6 (lina stori ndefu inakuja)!
“Kumbuka mwanzoni nilikuwa na boyfriend
ambaye tulipendana sana lakini hatukupanga kufunga ndoa. Nilimweleza
kila kitu akakubaliana na mimi japokuwa aliumia.
“Maskini! Kuanzia hapo nikawa nimeachana
na yule boyfriend wangu lakini hakukuwa na namna kwa sababu niliamini
nimepata mchumba wa kunioa.
ATAKIWA KUBADILI DINI
“Baadaye Dallas aliniambia nimeshakuwa
mchumba wake hivyo nibadili dini. Kweli nilibadili nikawa Muislam na
jina langu likawa Ilham. Hicho kilikuwa kipindi kigumu sana maishani
mwangu kwa sababu nilionekana ni muasi katika dini yangu ambayo mama ni
mzee wa usharika na mwimba kwaya, baba ni mtu wa kanisani sana.”
NINI KILIFUATA?
“Siku moja nilikuwa Tanga nashuti
filamu, nilikuwa nikitoka hapo niende Morogoro. Dallas alinipigia simu
akaniambia yupo Nairobi (Kenya) anakuja Tanzania. Nilimwambia nipo Tanga
akaniambia atanifuata kule. “Niliendelea kupiga mzigo. Zilipita saa
nyingi, baadaye nikiwa na kruu yangu, Dallas alinipigia simu akaniambia
ameniona.
“Nilikataa, akaniambia namna nilivyo, nguo nilizovaa na watu niliokuwa nao, alipatia. Kumbe alikuja na Toyota Prado.
WOLPER MORO, DALLAS DAR
“Tulipomaliza kurekodi Tanga tulikwenda
Morogoro, yeye aliniambia anaelekea Dar. Tulikuwa tunawasiliana.
Nilipomaliza kurekodi Moro nilirejea Dar. Hapo ndipo vituko vikawa juu
ya vituko.
“Niliambiwa mara kaonekana sehemu akiwa
na mwanamke au wanawake. Mimi sikujali kwa sababu nilipomuuliza
aliniambia hatuwezi kuonana kwa sababu kipindi hicho alikuwa katika
swaumu hivyo akionana na mimi nitamharibia. (ulikuwa mwezi mtukufu).
BADO HAWAJAKUTANA?
“(Mguno) Hapo bado hatujakutana lakini yupo mjini na amejaa tele kwenye kumbi za starehe.
“Baada ya kumaliza swaumu, siku moja
aliniambia anakuja nyumbani Mbezi Beach. Niliwaalika marafiki zangu
tukapika vyakula, tukafanya usafi na kufukiza udi chumbani. Nilitandika
mashuka meupe kitandani na kujipara kisha nikavaa ushungi kuanzia mchana
nikakaa kama malkia nikimsubiri mchumba.
“Huwezi amini, hadi giza linaingia
Dallas hakutia mguu. Nilipataje aibu kwa rafiki zangu waliotaka kumuona
huyo mchumba? Ninyi acheni tu!
“Nilipomuuliza aliniambia alipata dharura kuna biashara alikuwa anafanya
HATIMAYE WAKUTANA LAKINI…
“Nilikasirika sana, nikasema huyu ni
mchumba gani asiyetaka kuja kwangu? Nikampa muda wa siku tatu aje
nyumbani na alete nguo zake zote. Kweli, siku ya tatu, asubuhi
nilimsikia mtu akiita ‘Ilham Wolper Dallas’. Nilishajua sauti yake
kupitia simu hivyo nilimkaribisha na nguo zake nikaingiza ndani. Lakini
cha kushangaza alikuja na pikipiki!
“Alishinda nyumbani siku hiyo maana kuna
ndugu zake walikuja. Hatukufanya chochote. Dallas aliishia kunibusu
shavuni kisha jioni akaondoka.
“Mjini kukawa hakukaliki. Natumiwa picha
akiwa na wanawake tofautitofauti. Mmoja wa wanawake hao niliambiwa eti
ana ‘ngoma’! Jamani hii dunia ina kichaa!
“Muda ukasonga, vitimbi vikawa vingi.
Dallas simuoni. Muda wa kukaa kwenye ile nyumba uliisha hivyo nikahama
na nikamwambia akachukue nguo zake.
UCHUMBA WAVUNJIKA, SASA ANAPUMZIKA HAPA
“Baadaye uchumba ukavunjika tena mimi
ndiyo nilimwambia simtaki tena. Nilikaa muda hadi baadaye nilipopata
mwanaume wangu wa sasa. Anani-control vizuri kwa sababu kanipita umri na
ana busara. Tunapendana sana. Najuta kumfahamu Dallas. Siwezi kusahau
tukio hilo katika maisha yangu. Dallas alicheza na hisia za moyo wangu.
(akaangua kilio) Niliteseka sana. Ni Mungu tu anajua…
VIPI KURUDIA UKRISTO?
“Nimekaa muda siendi kanisani. Nilikuwa
najifungia ndani nalia kama mama yangu alivyokuwa anafanya. Siku moja
nilimwambia mwanaume wangu akaniambia kuliko kulia kila siku bora nirudi
kanisani. Ndipo nikarudia ukristo. Kwa sasa nasali Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kijitonyama, Dar,” alisema.
MBALI NA DALLAS
Kwa mara ya kwanza Wolper alikubali kuorodhesha listi ya wanaume aliowahi kuwa nao kimapenzi kwa kuwachambua mmoja mmoja.
ALI KIBA
Bila kupepesa macho, Wolper alikiri kuwa
msanii wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ndiye aliyemfundisha mapenzi: “Ni
kitambo kidogo. Wote hatukuwa mastaa lakini yeye alifanikiwa kuchomoka.
Kabla ya Ali (Kiba) nilikuwa na mwanaume lakini hatukuduu kwa maana ya
utu uzima, ilikuwa yale ya kitoto. Lakini Ali ndiye hasa aliyeniingiza
kwenye ulimwengu wa mapenzi.
KWA NINI WALIACHANA?
“Ali akawa staa. Alipokwenda nje
nikasikia wanawake wanamshobokea. Sasa mimi sikutaka karaha nikakaa
pembeni lakini jamaa ni mtu poa sana na tukikutana tunasalimiana freshi
kabisa.”
DIAMOND VIPI?
“Ni kweli niliwahi kuwa na Diamond
(msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul). Tulikuwa na uhusiano lakini pia
alikuwa mshirika wa kibiashara (hataki kuitaja). Yeye alikuwa hawezi
kulala bila kuniona, lakini tulikaa kama mwezi mmoja, kwa sasa amebaki
kuwa rafiki yangu na siyo mpenzi tena kama zamani,” alisema Wolper.
VIPI KUHUSU JUX?
“Jux (msanii wa Bongo Fleva, Juma
Khalid) nilikuwa naye kabla ya Dallas na yule mwanaume wangu
niliyeachana naye wakati wa Dallas. Katika maisha yangu nilimpenda sana
Jux. Siyo marioo ni mwanaume mtafutaji aliyejiamini. Kwa sasa sipo naye.
Dallas pia alichangia mimi kuachana na Jux,” alimalizia Wolper ambaye
kwa sasa ana mwanaume asiyependa kumwanika.
No comments:
Post a Comment