MSANII filamu na muziki wa kizazi kipya
wa Tanzania Baby Joseph Madaha maarufu kwa jina la (Baby Madaha) amesema
kwamba msanii mwenzake wa muziki nchini,Naseeb Abdul maarufu kwa jina
la Diamond Platinumz si msanii bali ni mfanyabiashara.
Madaha amesema kwamba Diamond si
mwanamuziki na kwamwe huwezi kumlinganisha na msanii kama Barnaba Boy,
anayefanya muziki kama sanaa na kazi kulingana na kipaji chake na kwamba
Diamond si msanii wa muziki bali ni msanii ngono anayefanya biashara ya
muziki kupitia mapenzi.
Baby madaha ambaye hivi sasa yuko nchini
Kenya kwa shuguli za muziki amesema kwamba, Diamond hajui kuimba na
ndiyo maana amekuwa msanii wa matukio huku nyota yake ikiegemea kwenye
mapenzi na wasichana wenye majina makubwa hususn wasanii.
Akizungumza na kandili yetu katika
mahojiano maalum leo baby Madaha alisema kwamba, “Binafsi niliposikia
kwamba Diamond anaumiza kichwa kunasa penzi la msanii Elizabeth Michael
maarufu kwa jina la (Lulu) sikushangaa hata kidogo. kwa sababu
nilitambua kwamba soko lake la muziki limeanza kushuka hivyo lazima
atafute eneo lingine la kujiimarisha kibiashara, ili jina lake liendelee
kuwika”.
“Siku wanawake maarufu nchini Tanzania
watakapo jitambua na kuacha kulewa penzi la Diamond ndiyo itakayokuwa
mwisho wa maisha yake kimuziki,kwa sababu hatakuwa na jipya na hivyo
soko lake litaanza kuporomoka”alifafanua Baby Madaha.
No comments:
Post a Comment