WOLPER, ZAMARADI BIFU ZITO!
Na Shakoor Jongo
STAA wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper amemrushia maneno ya lawama Mtangazaji wa Kipindi cha Take One, Zamaradi Mketema kuwa ni mnafki na adui yake mkubwa katika maisha.
STAA wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper amemrushia maneno ya lawama Mtangazaji wa Kipindi cha Take One, Zamaradi Mketema kuwa ni mnafki na adui yake mkubwa katika maisha.
Akizungumza na Amani juzikati, Wolper alisema amegundua kuwa mtangazaji huyo amekuwa akimfuatilia kwa karibu sana maisha yake kwa mtindo wa hasi (negative), akamuomba amuache.
“Nilibadili dini kutoka Ukristo kwenda Uislamu, Zamaradi akanifuatilia,
juzijuzi nimerudi kundini (kwenye Ukristo) kwa kusikiliza maneno ya
wazazi wangu, akanifuatilia tena.
“Huko
nyuma kupitia kipindi chake alikubali nidhalilishwe na waigizaji
wenzangu kwa faida yake (hakutaka kufafanua), iliniuma sana. Leo (hivi
karibuni) kaniweka hewani (kwenye redio) bila ya ridhaa yangu. Naomba
niseme kuwa naanza kugundua azma yake kwangu ni nini, aniache na maisha
yangu,” alilalama Wolper.
Baada ya Wolper kulalamika sana, Amani lilimtafuta Zamaradi kwa njia ya
simu ya kiganjani ambapo alisema yeye anawajibika kwa kazi yake hakuna
ishu ya kumfuatilia mtu.
“Mimi simfuatilii maisha yake, ni kazi tu. Kama mwandishi wa habari
nikipata habari ya mtu natakiwa kubalansi (uwiano) naye,” alisema
Zamaradi.Chanzop:www.globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment