“Umemwona Wema, kwa sasa ana ngozi nzuri yenye afya na iliyo
na mng’aro kama alivyokuwa awali,ni nzuri sana yani, ameacha kabisa
kutumia dawa za kung’arisha ngozi hilo ndilo lililonivutia zaidi kwani
alisikiliza ushauri niliompa kabla.”
Hiyo ni kauli ya staa aliyetikisa mwaka 2013 bwana Diamond Platnumz aliyoitoa hivi karibuni alipokuwa akizungumza na gazeti maarufu la michezo nchini hivi karibuni.
Diamond amesema Wema ndiye mwanamke anayetamani kuwa naye
katika maisha yake, hivyo kauli yake aliyoitoa mwanzo kuhusu kuzaa na
Wema ipo mbioni kutimia.
“Miezi kadhaa nyuma niliongea kuhusu nia yangu ya kuzaa na Wema, wakati huo nilikuwa bado na Penny,
siwezi kukimbia kivuli changu kwani ukweli unabaki palepale nampenda
yule binti, japokuwa wapo wanaosema kwamba sijatulia au natafuta ‘kiki’
kupitia warembo hawa, si kweli, Wema nilikuwa naye kabla ya Penny na
vigezo vyangu ni mchumba anayejali kazi yangu na kujua kwamba mimi ni
staa nahitajika sehemu yoyote, muda wowote, Wema ni mwelewa.” Alisisitiza Diamond
No comments:
Post a Comment