Translate

Sunday, March 17, 2013

KUMBE! KITALE ANGEOA SIKU MOJA NA MAREHEMU SHARO MILIONEA!


Wiki hii tunakutana na msanii wa Komedi na Bongo Fleva, Musa Yusuph ‘Kitale’. Hapa amefunguka juu ya uhusiano wake na marehemu Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ aliyefariki dunia Novemba, mwaka jana.
Funguka: Mambo vipi Kitale, shemeji yetu hajambo?
Kitale: (Kicheko kidogo) Hajambo, mzima wa afya, vipi!
Funguka: Moja kwa moja tuanzie kwenye uhusiano wako na marehemu Sharo Milionea, tunatambua alikuwa swahiba wako mkubwa, staili yenu ya maisha ilikuwaje?
Kitale: Kiukweli pengo la marehemu kwangu litabaki palepale. Tukiachilia mbali ushirikiano wetu kwenye kazi, alikuwa rafiki yangu mkubwa ndani na nje ya gemu. Tulisaidiana kwa mambo mengi sana, sidhani kama nitapata rafiki mwingine kama yeye. 
Funguka: Pole sana, mbali na huo ukaribu kuna kitu gani ambacho unakikumbuka na pengine kinakurudiarudia akilini mwako?
Kitale: (Akaongea kwa huzuni) Dah! tulikuwa na mipango mingi sana kuhusu muziki na maigizo tuliyokuwa tunayafanya, kubwa zaidi tulipanga kuoa kwa pamoja. ‘So’ nilivyopata habari za kifo chake, mipango yote iliharibika hadi nilipokuja kujipanga upya. Tukio hilo hujirudia sana akilini mwangu.
Funguka: ‘Anyway’, ndoa yako ilikuwa wazi na kila mtu anamjua shemeji, unaweza kututajia hata jina la huyo aliyekuwa mtarajiwa wa marehemu?
Kitale: Mh! Hapana labda siku mwenyewe akiniruhusu kumtaja nitafanya hivyo. 
Funguka: Watu wanasema wewe ndiye mrithi wa Sharo Milionea, unazungumziaje ishu hiyo?
Kitale: Dah! Nilikuwa sijui, ila mimi sioni tatizo ingawa kwa upande wangu naona kama tulikuwa na ladha tofauti, japo tuna wasifu unaofanana.
Funguka: Kitale tunashukuru kwa ushirikiano wako, kazi njema.
Kitale: Nashukuru, tuchekiane ‘next time’.

No comments: