Tuesday, July 24, 2012

ODAMA ::MDOGO MDOGO NDIO MWENDO


Msanii huyo ni mmiliki wa Kampuni ya J-Film 4 Life Production, alisema kwamba kuna mambo kadhaa ameamua kuyaweka kwanza sawa.

Ni yule Mwigizaji na Mtayarishaji wa Filamu nchini, Jennifer Kyaka ‘Odama’ alisema kwa sasa anajipanga kwanza na hataweza kununua muswada ‘Script’ hadi hapo mapema mwakani.

Nia na dhumuni la msanii huyo kuanzisha kampuni yake ni, ilikuwa kuhakikisha anatoa kazi iliyokuwa bora na sio kulipua na hiyo itamsaidia kufanya vyema sokoni na kuweza kurudisha hata zile gharama za matengenezo.

Mbali na hilo msanii huyo hupokea kazi za wasanii wengine na kuzitengeneza, alidokeza mbali na hilo amekuwa akiwashauri hata wasanii wengine wanaotengeneza kazi kwake watoe kazi zenye ubora ambazo zitajikita zaidi kufunza, kuelimisha na kuiasa jamii zaidi ya kuburudisha.

No comments:

Post a Comment